Masala afungua mafunzo ya mgambo ilemela

MWANZA :Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amefungua rasmi mafunzo ya Jeshi la akiba (MGAMBO) katika viwanja vya Lumala Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza huku akisisitiza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani yanawafanya vijana kuwa wazalendo kwa Taifa lao.
“Mafunzo haya yanawatengeneza na yatawawezesha kijitegemea,kuwa wazalendo na kupambana na mazingira yenu kwa hali zote.”…Amesema
Kwa upande wake Luteni kanali Evans Akili ambaye ni Mshauri wa Jeshi la akiba Wilaya ya Ilemela ameeleza umuhimu wa mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na vijana wanaohitimu kuwa chachu ya ulinzi na usalama ndani ya jamii na Taifa lao kwa ujumla.
Tutaendelea kuwanoa vijana hawa wawe wazalendo kweli kweli na wawe bidhaa adhimu yenye manufaa kwa nchi yetu.”..amesema
Jumla ya wanafunzi 97 wa mafunzo ya askari wa akiba wamejiandikisha mwaka huu 2023 ndani ya Wilaya ya Ilemela ambapo mafunzo hayo yatachukua miezi mitatu hadi kutamatika kwake.

Habari Zifananazo

Back to top button