Masasi mambo safi huduma za afya Mtandi

WANANCHI wa Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara wameeleza kufurahishwa na upatikanaji wa huduma za afya katika Kata ya Mtandi, wilayani Masasi.

Huduma hizo zimeanza kutolea baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.

Kituo kimesaidia kupunguza adha kwa wananchi kutembea umbali mrefu kupata huduma za afya wilayani Masasi.

Kituo hicho chenye vifaa vya kisasa kimeanza kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya 30,000 kutoka ndani na nje ya Kata ya Mtandi, baada ya ujenzi wake kukamilika Januari 2023.

Mkurungezi Mtendaji wa Wilaya ya Masasi, Erica Yegella amesema kituo hicho kimejengwa na serikali kwa gharama ya shilingi milioni 500.

“Kituo cha Afya Mtandi kimejengwa na serikali na sasa kimekamilika na kuanza kutoa huduma za afya Kwa wananchi,” amesema Yegella na kuongeza kuwa kituo hicho kina vifaa bora na vya kisasa, ambavyo vimenunuliwa na serikali kwa shilingi milioni 150.

Amesema wananchi zaidi ya 30,000 kutoka ndani ya Mtandi na maeneo ya jirani ya Kata za Mkuti, Jida, Napupa, Marika na Chanika wanapatiwa huduma za afya kupitia kituo cha Mtandi.

Habari Zifananazo

Back to top button