Waziri wa Mambo Ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewateua Jaji Mstaafu John Mgeta na Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Ally Malewa kuwa wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa siku ya leo Julai 13, 2023 na kitengo cha mawasiliano serikalini, wizara ya mambo ya ndani ya nchi, uteuzi huo unakamlisha wajumbe wa bodi hiyo baada ya baadhi ya wajumbe wa awali kumaliza muda wao.
Mwezi Aprili mwaka 2023 Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Balozi Khamis Sued Kagasheki kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo na kufanya bodi hiyo kuwa na wajumbe sita.
Aidha taarifa hiyo iliwataja wajumbe hao kama, Camilius M. Wambura (IGP) , Mganga mkuu wa serikali, Prof Tumaini Nang, Coletha Kiwale, Sylvester Mwakitabu, Ramadhani Mnyaka na Balozi Khamis Kagasheki.