Masauni, wakuu wa vyombo vya usalama wateta
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Vyombo vya Usalama na Watendaji wa Ununuzi na Ugavi wa Wizara yake katika kikao kazi kilichofanyika Ofisi ndogo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam, leo Januari 23, 2024.
Katika Kikao hicho pia alishiriki Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kaspar Mmuya, pamoja na Wakuu wa vyombo vya Usalama vyote vya Wizara ambavyo ni Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji, kilijadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi katika masuala ya ulinzi na usalama.