Mashahidi 14, vielelezo 17 kesi ya Dk Pima

MASHAHIDI 14 na vielelezo 17, vinatarajiwa kutolewa na upande wa Jamhuri katika kesi ya ubadhirifu inayomkabili, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake watatu.

Mbali ya Dk Pima watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Fedha na Uchumi, Mariam Mshana, aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango na Uchumi, Innocent Maduhu na Mtumishi wa Jiji idara ya fedha, Alex Daniel.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule, alisema mahakamani leo kuwa wanatarajia kuwa na mashahidi 14 na vielelezo 17 katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Fadhil Mbelwa, ambapo washitakiwa wanatetewa na Wakili Sabato Ngogo.

Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka sita ikiwemo ufujaji na ubadhirifu.

Habari Zifananazo

Back to top button