Mashahidi 24 kutoa ushahidi kesi ya Saitoti

MASHAHIDI 24 wanatarajiwa kutoa ushahidi na kuwasilisha vielelezo 11 katika kesi ya shambulio la kudhulu mwili na kukaidi amri ya Wizara ya Madini inayomhusu mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, Joel Mollel “Saitoti” na wafanyakazi wake sita.

Akiwasomea maelezo ya awali watuhumiwa hao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara , mwendesha mashitaka wa serikali, Mosses Hamilton alisema kesi hiyo itawasilisha vielelezo 11 na mashahidi 24 katika Kesi mbili zinazowakabili wafanyakazi wa Kampuni ya Gem & Rock Venture inayomilikiwa na Saitoti kwa kuchimba Mgodi uliopo Kitalu B Mirerani.

Hamilton alidai katika kesi ya shambulio inawahusu washitakiwa sita akiwemo Petro Exsaud 48 mkazi wa Moshono Arusha, Mosses Kelerwa 45, mkazi wa Mirerani,Daniel Siyaya 44, mkazi wa Ilboru Arusha, Mosses sirikwa 46, mkazi wa Ilboru, Dausen Mollel 58, Mkazi wa Ilboru na, Enock Nanyaro32 mkazi wa Arusha kesi hiyo itakuwa na mashahidi 16 na vielelezo sita.

Mwendesha mashitaka huyo alidai katika shtaka lingine la kukaidi amri ya wizara linalomkabili Saitoti na Nanyaro litakuwa na mashahidi 8 na vielelezo 5 na mashahidi wanahifadhiwa hadi mei 10 kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa katika mahakama hiyo.

Katika maelezo ya awali ,Hamilton alidai kuwa Machi 13 mwaka huu wafanyakazi sita wa Gem & Rock Venture waliwashambulia kwa majabali na vifaa vya uchimbaji watumishi wa Taasisi kadhaa za serikali na wafanyakazi sita wa Kampuni ya Franone inayochimba Kitalu C akiwemo Benson Banash ,Vedastus Swea,Alvin Msuya,Swetbert Albogast,Mussa Unambe na Bonfance Mollel na kuwapatia majeraha makubwa usoni

Hamilton alidai kuwa washitakiwa hao walitenda kosa Hilo wakati wakijua wazi kuwa kufanya kosa hilo ni kosa kisheria lakini washitakiwa wote walikana maelezo ya awali na dhamana yao iliendelea kwani kila mshitakiwa alidhaminiwa na mdhamini mmoja na Bondi ya shilingi milioni moja

Katika Kesi nyingine maelezo ya awali ya washitakiwa hao wawili Saitoti na Nanyaro mwendesha mashitaka Hamilton ilidaiwa wameshitakiwa kwa shitaka moja la kukaidi amri ya Wizara ya Madini ya ambapo ilidaiwa kuwa walizuiwa kufanya shughuli za uchimbaji baada ya mtobozano na Kitalu C lakini walikaidi kwa maandishi na kuendelea na kazi wakati wakijua wazi ni kosa kisheria kuzuia agizo la serikali.

Washitakiwa walikana shtaka hilo na dhamana ya mtu mmoja mmoja iliendea na kesi ilihairishwa hadi mei 10 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa rasmi.

Habari Zifananazo

Back to top button