Mashauri 333 yamalizwa nje ya mahakama

TANGA: Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imefanikiwa kumaliza jumla ya mashauri 333 nje ya Mahakama katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu

Hayo yamesemwa Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Boniphace Luhande wakati wa ufunguzi wa baraza la pili la wafanyakazi wa ofisi hiyo lililofanyika jijini Tanga

Amesema kuwa utaratibu wa mashauri kabla ya kuyafikisha mahakamani umesaidia kupunguza wingi wa mashauri kwenye mahakama, lakini na kupunguza muda wa kuendesha madai hayo.

Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2022/23, ofisi hiyo imeokoa zaidi ya Sh Bil 609.3, ambazo zingelipwa kwa wadaawa, endapo serikali ingeshindwa kwenye mashauri mbalimbali.

Naye Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo, Mark Mulwambo amesema kuwa baraza hilo limekuwa kiungo muhimu cha ushirikiano na uhusiano mzuri kazini baina yake na wafanyakazi.

“Malengo makuu ya mwaka huu licha ya kuiwakilisha serikali na taasisi zake katika mashauri ya ndani na nje ya nchi ni kuhakikisha tunakuwa na watumishi wenye kufanya kazi kwa ufanisi na weledi mkubwa,”amesema Mulwambo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x