Mashindano Lake Manyara yaiva

ARUSHA;MASHINDANO ya riadha ya Lake Manyara Marathon yamepangwa kufanyika  Oktoba 29  mwaka huu, yakilenga kutangaza utalii na kuibua vipaji vya riadha nchini.

Wanariadha 3000 wanatarajiwa kushiriki mbio hizo zitakazofanyika kwa mara ya kwanza katika mji wa Mto wa Mbu, Wilaya Monduli Mkoa wa Arusha.

Mwanariadha wa kimataifa, Emmanuel Giniki, ameteuliwa kuwa Balozi wa mbio hizo, na ni  miongoni mwa washiriki wa Lake Manyara Marathon.

Makundi mbalimbali ya wanariadha kwa wanawake na wanaume yatahusika katika mbio za Kilometa 21, kilometa 10 na kilometa 5.

Mkurugenzi wa kampuni ya Greenleaf Mohar, ambao ndio waandaaji, Morris Okinda amesema mbio hizo zitaenda kufanyika kwa mara kwanza zikilenga kuibua na kutangaza utalii wa hifadhi ya Ziwa Manyara.

“Lengo ni kupata wachezaji watakaowakilisha taifa kimataifa na tunatarajia kuwa na taasisi ya ‘Posso International Sports’ kutoka Marekani, ambao watafika nchini kuangalia vipaji na hii itafungua fursa ya vijana kuonekana na wanariadha wetu wataweza kuwakilisha nchi wakiwa na kiwango cha  kimataifa,”ameongeza Okinda.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
AnneSmith
AnneSmith
2 months ago

Earn income while simply working online. work from home whenever you want. just for maximum 5 hours a day you can make more than $600 per day online. From this I made $18,000 last month in my spare time.
.
.
Detail Here——————————————————>>>  http://Www.BizWork1.Com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x