Mashindano ya mbuzi kusaidia jamii Dar

Mashindano ya mbuzi kujenga vyoo, kukarabati madarasa

KIASI cha Sh milioni 70 kitatumika kuboresha huduma za elimu kwa kujenga miundombinu kama vyoo na ukarabati wa madarasa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam, Meneja Mradi wa Klabu ya Rotary ya  Oysterbay, Mathew Hellela, amesema kupitia mashindano ya mbio za mbuzi yatakayofanyika Novemba 5, 2022 viwanja vya The Green vilivyoko Oysterbay, watachanga fedha hizo kupitia wafadhili na watu wengine.

“Huu ni mwaka wa tatu kufanya mbio hizi kwa jina la The Goat Races na kwa mwaka huu zitaendeleza dhumuni kuu, ambalo ni shughuli ya furaha kwa familia, ambayo mapato yake yataelekezwa katika miradi ya kijamii,”ameeleza Hellela.

Advertisement

Amesema fedha za kwenye mbio hizo pia zitatumika kuzingatia maeneo muhimu sita yaliyopewa kipaumbele, ambavyo ni  miradi mipya na yanayondelea kama utoaji vifaa na elimu ya usafi.

Maeneo Mengine aliyoainisha ni amani na usuluhishi wa migogoro, kujikinga na kutibu maradhi, maji na usafi, afya ya wajawazito na watoto, elimu ya msingi, uchumi na maendeleo ya jamii.

Amebainisha kuwa hadi sasa wadhamini mbalimbali wamejitokeza ambao ni Pepsi, Amici Design, Freixene, TBL, Automark, Toyota, Oryx Energies,The Tanzanite Dream, Smile, East Africa Radio, SCHNU”S

Advertising Dar na Hotel Slipway.