Mashindano ya mbuzi kukusanya Sh Mil.100

RAIS wa Rotary Klabu ya Oysterbay, Dar es Salaam ,Krutin Shah, amesema wanatarajia kukusanya kiasi cha Sh milioni 100, ili kusaidia kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, alisema mashindano ya mbio za mbuzi yatafanyika Novemba 5, 2022 katika viwanja vya The Green vilivyoko Oysterbay na watachanga fedha hizo kupitia wafadhili na watu wengine.

Amesema fedha za kwenye mbio hizo zitatumika kuzingatia maeneo muhimu sita yaliyopewa kipaumbele, ambao ni  miradi mipya na inayoendelea kama misaada ya elimu, utoaji vifaa na elimu ya usafi.

Maeneo mengine aliyoainisha ni amani na usuluhishi wa migogoro, kujikinga na kutibu maradhi,maji na usafi ,afya ya wajawazito na watoto, elimu ya msingi, uchumi na maendeleo ya jamii.

“Kama ilivyo katika miaka iliyopita, mbio hizi za mbuzi zimeweza kuvutia wadhamini  wengi na mwaka huu hatutakuwa na tofauti, tunashukuru kwa uaminifu tuliopewa na wadhamini wetu katika uwezo wa utayarishaji huu,” amesema.

Kwa upande wake Meneja Mradi, Mathew Hellela, ameeleza kuwa tamasha hilo litakuwa na burudani ya kutosha na vionjo mbalimbali vya kumfurahisha kila mtu.

Amesema tiketi ya kawaida kwa mtu mzima ni Sh 15,000 na watoto Sh 5000, huku VIP ikiwa ni Sh 180,000  na Sh 3000 kwa watoto

 

Habari Zifananazo

Back to top button