RASMI: Yanga imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo Pacôme Zouzoua kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Yanga imetangaza usajili huo muda huu kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Zouzoua amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumika klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani.
Mchezaji huyu msimu uliopita alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya nchi hiyo.