Mashirika 16 ya Umma yaunganishwa, manne yafutwa

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa nchi, ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa, Kitila Mkumbo amesema Serikali imeridhia na kuelekeza kuunganishwa kwa mashirika na taasisi 16 ambazo majukumu yake yanashabiana na kufuta Mashirika na Taasisi za Umma nne ili kuongeza tija ya uendeshaji na kukuza Maendeleo.

Waziri MKUMBO amesema tayari Serikali iliunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kina kuhusu utendaji wa mashirika ya umma kwa lengo la kubainisha changamoto za kiutendaji na kupendekeza hatua za kuchukua katika kuongeza tija ya maendeleo ya nchini.

Aidha amesema Mashirika na Taasisi za Umma zilizofutwa ni Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi (Tanzania Police Force Corporation Sole -TPFCS) ,Taasisi ya Chakula na Lishe (Tanzania Food and Nutrition Centre – TFNC), Shirika la Elimu Kibaha (Kibaha Education Center – KEC) pamoja na Bodi ya Pareto ambapo shughuli zake zitahamishiwa katika Mamlaka ya Usimamizi wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko.

Advertisement

Sambamba na hayo amewatoa hofu wafanyakazi wote katika mashirika na taasisi hizo kuwa hakuna mtumishi atakayepoteza ajira yake na kwamba maslahi yote ya watumishi ya umma yatalindwa na kuzingatiwa kikamilifu kwa kufuata sheria na kanuni za utumishi wa umma.

Mashirika na Taasisi za umma zinazounganishwa ni pamoja Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (National Identification Authority-NIDA) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Registration, Insolvency and Trusteeship Agency -RITA) ambapo yameunganishwa na kuunda taasisi moja inatayohusika na utambuzi wa matukio muhimu maishani,Benki ya Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Development Bank -TADB) na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (Agricultural Inputs Trust Fund -AGITF) ambapo zimeunganishwa ili kuwa na taasisi moja itakayohusika na mikopo na ugharamiaji wa maendeleo ya kilimo nchini.

2 comments

Comments are closed.