Mashirika 7 yasaini mikataba kinyume cha sheria

MASHIRIKA saba ya umma yamesaini mikataba ya Sh bilioni 45. 71 na Dola milioni 7.75 bila kupekuliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) au ofisa sheria kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza.

Akiwasilisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, CAG Charles Kichere, amesema kitendo hicho ni kinyume na sheria za ununuzi wa umma, ambayo inahitaji mkataba wowote rasmi ambao thamani yake ni zaidi ya Sh bilioni 1 kuhakikiwa na mwanasheria mkuu wa serikali kabla ya kusainiwa na wahusika.

Amesema kutohakikiwa kwa mikataba hiyo na mwanasheria mkuu wa serikali kunaweza kusababisha migogoro ya kimkataba na kisheria katika utekelezaji wa mikataba hiyo.

“Napendekeza mashirika ya umma yazingatie ushauri wa sheria katika mikataba, ili kuepuka migororo na hasara zinazoweza kutokea kisheria, pia mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma ichukue hatua kwa mashirika yanayosaini mikataba mikubwa bila kuhakikiwa na mwanasheria mkuu wa serikali,”amesema CAG Kichere.

Habari Zifananazo

Back to top button