Mashirika ya umma kuimarika sheria ya ununuzi

SERIKALI leo Septemba 7, 2023 imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023, huku ikiainisha matokeo mbalimbali kutokana na kutungwa kwa sheria hiyo.

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba ametaja matokeo hayo ni pamoja na kuimarika kwa mazingira ya ununuzi na ugavi kwa taasisi na mashirika ya umma yanayojiendesha kibiashara.

Ametaja matokeo mengine kuwa ni kujumuisha katika mnyororo wa ugavi masuala ya ununuzi, ugavi na uondoshwaji wa mali kwa njia ya zabuni ili kupata thamani halisi ya 3 fedha zinazotumika kupitia ununuzi na utekelezaji wa miradi ya Serikali.

“Kuimarika kwa usimamizi wa mikataba ya ununuzi, kuongeza ufanisi katika mnyororo wa ugavi kupitia matumizi ya mfumo wa ununuzi kwa njia ya kielektroniki kwenye ununuzi, ugavi na uondoshwaji wa mali kwa njia ya zabuni.

“Kuweka masharti ya bei kikomo kwa baadhi ya bidhaa na huduma katika ununuzi wa umma na hivyo kudhibiti gharama, kuongezeka kwa ufanisi katika utekelezaji wa miradi kwa utaratibu wa force account, kupunguza urasimu katika uidhinishaji wa zabuni hivyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za mnyororo wa ugavi; na kufuta Sheria ya Ununuzi wa Umma, Na. 7 ya mwaka 2011,” amesema Waziri wa Fedha.

Habari Zifananazo

Back to top button