Mashujaa waichinja Simba Kigoma

KIGOMA: MASHUJAA FC imekata tiketi ya kucheza hatua ya Robo Fainali ya Kombe La Shirikisho la CRDB baada ya kumfunga mnyama Simba SC kwa penalti 6-5 baada ya dakika 90′ za mchezo kutamatika kwa sare ya 1-1.

Bao la mapema la Leriant Lusajo dakika 5′ likawafanya Mashujaa kwenda mapumziko wakiwa wababe wa mchezo.

Kipindi cha pili, Simba SC ikafanya mabadiliko yaliyowapa tija kwa kumuingiza Fredy Michael aliyeisawazishia timu yake dakika ya 51′.

Dakika 90′ zikatamatika kwa sare ya 1-1 hivyo kugeukia hatua ya changamoto ya mikwaju ya penalti.

Waneni, hunena historia hujirudia, mnamo Machi 21, 2021 Mashujaa wakiwa katika Ligi Daraja la Kwanza waliitoa Simba SC katika michuano hiyo kwa mabao 3-2 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button