TIMU ya Mashujaa ya Kigoma imeanza vyema mchezo wake wa mtoano wa kutafuta tiketi ya kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Mashujaa wakiwa nyumbani katika dimba la Lake Tanganyika wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City, hivyo kuikaribia Ligi Kuu msimu ujao.
Kocha mkuu wa Mashujaa FC, Abdul Mingange amesema licha ya ushindi huo bado kazi haijaisha.
“Soka ni mchezo wa maajabu sana ,kwa mtizamo wangu bado kazi haijasha, tumemaliza nusu ya kwanza bado nusu ya pili kule sokoine,”amesema Mingange.
Kwa upande wake Kocha msaidizi wa Mbeya City, Paul Nonga amesema wamejifunza kutokana na mchezo wa leo na haijasha mpaka iishe kabisa.
” Tumefanya makosa ambayo wenzetu wameyatumia tunakwenda kujipanga katika dimba la Sokoine, lolote linaweza kutokea katika mpira,” amesema Nonga.
Mchezo wa mkondo wa pili utapigwa kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya Juni 22 na mshindi wa jumla atacheza Ligi Kuu msimu ujao.