Masista wafurahishwa maono chanya Polisi

KILIMANJARO; Masista kutoka Shule ya Mtakatifu Maria Goreti ya mjini Moshi, wamesema kwa sasa Jeshi la Polisi limekuwa likionekana kuanza kubadilika katika utendaji kazi wao, huku wakibainisha kuwa endapo mabadiliko hayo yakIendelea imani kwa wananchi itakuwa kubwa zaidi kwa jeshi hilo.

Hayo wameyabainisha walipofika Shule ya Polisi Tanzania kuhudhuria hafla ya kuvishwa nishani maofisa na wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali iliyofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.

Pia walizungumza na Mkuu wa Mawasiliano katika Shule ya Polisi Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Angela Kibiriti na kupata maelezo mafupi ya shule hiyo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button