Masomo yaongezeka mtaala mpya msingi

TAASISI ya Elimu Tanzania imetoa mtaala wa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba 2023.

Muundo wa mtaala huo umebadilika na sasa elimu hiyo itakuwa ni ya miaka sita badala ya saba kama ulivyokuwa Mtaala wa Elimu ya Msingi wa mwaka 2016.

Mtaala huo umezingatia nadharia za ukuaji na ujifunzaji na falsafa ya elimu ya kujitegemea inayosisitiza elimu inayomwezesha Mtanzania ajitegemee na amudu maisha yake ya kila siku.

Muundo wa mtaala unaonesha elimu ya msingi itatolewa kwa miaka sita katika hatua mbili ambazo ni darasa la kwanza na la pili ili kujenga umahiri katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Katika hatua ya pili inaonesha mtaala huo utaanzia darasa la tatu hadi la sita na italenga kuimarisha stadi za KKK na stadi nyingine za maisha.

Mwanafunzi wa shule ya msingi anatakiwa aanze darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka sita na kumaliza darasa la sita akiwa na umri wa miaka 11.

Kwa mujibu wa mtaala huo mwaka wa masomo utakuwa na siku 194 sawa na wiki 39 na umegawanyika katika mihula miwili inayolingana.

Katika kila muhula wiki mbili zitatumika kwa ajili ya upimaji endelevu na tamati.

Vipindi na muda wa ufundishaji na ujifunzaji katika elimu ya msingi utakuwa dakika 30 kwa kila kipindi kwa darasa la kwanza na la pili na dakika 40 kila kipindi kwa darasa la tatu hadi la sita.

Katika eneo la Dira, Malengo na Umahiri wa Jumla, mtaala umelenga kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi na mitazamo chanya, anayethamini usawa, haki na elimu bila ukomo katika kuleta maendeleo endelevu ya kitaifa na kimataifa.

Kwa mujibu wa mtaala huo, maeneo ya kujifunza na umahiri mkuu kwa darasa la kwanza na la pili yamezingatia ujenzi wa lugha, mawasiliano na stadi za hisabati, utamaduni, sanaa, michezo na afya na mazingira.

Kwa darasa la tatu hadi la sita maeneo ya kujifunza na masomo yamezingatia kumjengea mwanafunzi umahiri wa lugha na mawasiliano, hisabati, sayansi ya jamii, sayansi na teknolojia na sanaa na michezo.

Katika eneo la lugha wanafunzi hao watajifunza masomo ya lugha za Kiswahili, Kiingereza, Kichina, Kiarabu na Kifaransa.

Mtaala umeelekeza kuwa katika eneo la sayansi ya jamii watakuwa na masomo ya historia ya Tanzania na maadili, Jiografia na mazingira, hisabati, sayansi, sanaa na michezo.

Aidha, lugha ya kufundishia kwa mujibu wa mtaala huo Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 inaelekeza matumizi ya lugha ya Kiswahili, Kiingereza, Lugha ya Alama Tanzania (LAT) na lugha nyingine za kigeni katika elimu na mafunzo.

Sera inatamka kuwa lugha ya Kiswahili itatumika kama lugha ya kufundishia katika shule zinazotumia Kiswahili na Kiingereza kitatumika katika shule zinazotumia Kiingereza kama lugha ya kujifunzia na kufundishia.

Aidha, masomo ya lugha za Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kichina na Kiarabu yatafundishwa kwa lugha inayohusika.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Lyabwene Mtahabwa mtaala huo umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023.

Dk Mtahabwa pia alieleza kuwa mtaala umezingatia maoni ya wadau yaliyokusanywa na kuchakatwa kati ya mwaka 2021 na mwaka jana na matokeo ya uchambuzi wa maandiko kuhusu uzoefu kutoka nchi nyingine.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
9 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Najma
Najma
1 month ago

huyu demu aliyecheza na diamond JEJE ANAPATIKANA MKOA GANI ANATAFUTWA… TUMPE MAUA YAKE ANASTAHILI KUWA NA WAJUKUU 90

OIP.jpeg
Last edited 1 month ago by Najma
zurdeherdi
zurdeherdi
Reply to  Najma
1 month ago

My first payment is $27,000. I’m thrilled since this is the first time I’ve truly earned stuff. From this point on, I’m going to work even harder, and I can’t wait till the next vs10 week to get paid. Click the home tab to find out more.
.
.
Using Here————————————>>> https://Fastinccome.blogspot.Com/

yirzoharde
yirzoharde
1 month ago

Mkoa wa Mbeya limewajulisha vijana waliotuma maombi ya kujiunga na jeshi hilo kutembelea mbao za matangazo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,

MAPINDUZI.GIF
yirzoharde
yirzoharde
1 month ago

Mkoa wa Mbeya limewajulisha vijana waliotuma maombi ya kujiunga na jeshi hilo kutembelea mbao za matangazo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

MAPINDUZI1.GIF
Chukua Mkifo huooo
Chukua Mkifo huooo
1 month ago

Matokeo yanaonesha ya Majengo+Mlinzi yanayotakiwa kusikimikwa viwanda/ viliyofunguliwa zamani ni 455,789 vinasubiri wawekezaji wapya kabisa kutoka labour

Matokeo yanaonesha kuwa, katika jumla ya viwanda vyote 49,243 (vikubwa na vidogo) vilivyohusika katika Sensa ya Uzalishaji Viwandani kwa mwaka 2013.

MAPINDUZIII.GIF
Erick
Erick
1 month ago

Mtaala

Erick
Erick
1 month ago

Mtaala huu hauna somo la historia ya Afrika kwa nn?
Je, hatutaki kujua wenzetu walifanya nn kufikia hapo walipo?

Nisaidien nielewe maana yake nn

Issakwisa Gideon mwasanjobe
Issakwisa Gideon mwasanjobe
1 month ago

Tatizo la nchi yetu tunakwama kwasababu tunafuata nchi nyingine walivyofanikiwa badala ya kufuata mipango yetu Mizuri tuliopanga na Ili tuendelee Toka uhuru

Dominick
Dominick
1 month ago

Nivizuri kuwa na mipango Kama hiyo ilikuweza kujua tunaweza au hapana

Back to top button
9
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x