TEHRAN: MWANAMAGEUZI Dk Masoud Pezeshkian amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran akimshinda mpinzani wake mwenye msimamo mkali, Saeed Jalili katika uchaguzi wa Rais.
Dk Pezeshkian amechaguliwa baada ya kupata asimilia asimilia 53.3 ya zaidi ya kura milioni 30 zilizohesabiwa. Jalili amepata asilimia 44.3.
Uchaguzi wa maurudio umefanyika baada kutopatikana mshindi wa wingi wa kura katika awamu ya kwanza Juni 28, ambao ulishuhudia idadi ndogo zaidi ya wapiga kura kuwahi kutokea ya asilimia 40.
Soma hapa: http://Rais wa Iran afariki dunia
Uchaguzi huo uliitishwa baada ya aliyekuwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi kufariki pamoja na watu wengine nane katika ajali ya helikopta Mei mwaka huu.
Hata kabla ya matokeo ya mwisho kutangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran, wafuasi wa Dk. Pezeshkian walikuwa tayari wametoka mitaani jiji Tehran na miji mingine kadhaa kusherehekea.
Mitandao ya kijamii ilionyesha watu hasa vijana wakicheza na kupunga bendera ya kijani ya kampeni yake, huku magari yakipiga honi.
Dk. Pezeshkian, daktari wa upasuaji wa moyo mwenye umri wa miaka 71 na mwanachama wa bunge la Iran, ni mkosoaji wa polisi wa maadili wa Iran na alileta msisimko baada ya kuahidi umoja na mshikamano, pamoja na kumaliza kutengwa kwa Iran katika Jumuiya ya Kimataifa.
Pia ametoa wito wa mazungumzo yenye kujenga na mataifa yenye nguvu ya Magharibi kuhusu kurejewa kwa majadiliano ya nyuklia wa 2015 uliokwama ambao Iran ilikubali kuachana na mpango wake wa nyuklia kwa kurudishiwa unafuu wa vikwazo vya Magharibi.
Mpinzani wake, Saeed Jalili, anaunga mkono hali ilivyo. Ni mjumbe wa zamani wa mazungumzo ya nyuklia anayeungwa mkono na jamii za kidoni zenye nguvu zaidi za Iran.
Jalili anajulikana kwa msimamo wake mkali wa kupinga Magharibi na kurejeshwa kwa makubaliano ya nyuklia, ambayo anasema yalivuka mipaka.
Ushiriki wa wapiga kura katika raundi ya hivi karibuni ya kupiga kura ulikuwa asilimia 50 zaidi kuliko raundi ya kwanza wiki iliyopita uliolikuwa wa chini zaidi tangu mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979.
Kutojitokeza kwa wingi kwa wapiga kura kulimaanisha kwamba mamilioni ya watu waligomea uchaguzi.
Ripoti zimesema baadhi ya watu ambao hawakupiga kura katika raundi ya kwanza walishawishiwa kupiga kura kwa Dk. Pezeshkian katika uchaguzi wa marudio ili kumzuia Jalili asiwe Rais.
Walihofia kuwa kama angechaguliwa, Iran ingeendelea kukabiliana na ulimwengu wa nje na angeleta vikwazo zaidi na kutengwa zaidi kwa Iran.