Matibabu ya kibingwa kuboreshwa

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kununa vifaa vya matibabu ili huduma nyingi za kitabibu au matabibu bingwa zitolewe nchini.

Rais Samia amesema serikali imeshajenga hospitali , vituo vya afya na zahanati za kutosha na kazi iliyobaki ni kutengeneza watumishi watakaotoa huduma kwa wananchi.

Akizungumza leo Machi 19, 2023 katika maadhimisho ya miaka miwili ya urais wake, Rais Samia amezungumzia mpango wa M-mama kuwa una nia kunusuru maisha ya mama wakati wa kujifungua .

Rais samia amesema mpango huo umepata sifa duniani kote na sasa mashirika mbalimbali ya kimataifa wanakwenda kutekeleza mradi huo katika nchi mbalimbali huku Tanzania ikiwa tayari imeshaanza.

“Ni mpango kabambe umepata sifa duniani kote na sasa mashariki mbalimbali kimataifa wanakwenda kuutekeleza mradi huu katika nchi mbalimbali lakini Tanzania tumeanza”.amesema Rais Samia.

Habari Zifananazo

Back to top button