Matinyi: Ruksa waandishi kutoa taarifa za Serikali

DODOMA: Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amesema ni ruksa kwa Vyombo vya Habari vya kujitegemea na Waandishi wa Habari kutoa taarifa na matangazo yanayohusu Serikali akisisitiza takwa hilo ni kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari Sura 229 na Marekebisho yake ya Mwaka 2023.
Matinyi amesema baada ya taarifa kuenea mitandaoni zikiihusisha Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro ikisema ni kosa kisheria kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (1) (b), (iv) cha Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kwa Chombo cha Habari binafsi au Mwandishi wa Habari kuzungumza masuala mbalimbali ya Serikali (National Issues) bila idhini au mwongozo wa Serikali.
“Hilo siyo sahihi,” amesema Matinyi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. “Sheria imeweka bayana haki za msingi za Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari ambazo ni kutafuta, kuchakata na kutangaza au kuchapisha habari. Waandishi wanaruhusiwa isipokuwa kwa taarifa ambazo zimezuiliwa kwa mujibu wa Sheria.”

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button