Matokeo yawakera wachezaji Simba

NAHODHA  wa Simba John Bocco, amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wameumizwa pia na matokeo waliyopata katika michezo iliyopita na kufifisha matumaini yao ya kunyakua taji lolote msimu huu.

Bocco anasema wachezaji wa Simba wanatamani kushinda mataji, hivyo inapotekea wanakosa kutimiza malengo wanaumia, lakini amewataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono, kwani watapambana kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyosalia, ili kuwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo.

“Tuna viongozi thabiti wameona changamoto zilizotukwamisha msimu huu, ninaamini watafanyia kazi mapungufu hayo ili kuwa na msimu bora unaokuja, tunapitia nyakati za mpito ambazo zitapita,” amesema.

Simba wanajiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Ijumaa wiki hii Uwanja wa Azam, Chamazi, Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button