Matola: Simba Vs Tabora United haitakua rahisi

TABORA: KOCHA Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola amesema kuwa kuelekea mechi yao ya kesho dhidi ya Tabora United haitakua mechi nyepesi licha ya kupata ushindi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma, uliochezwa mwishoni mwa juma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, mkoani Kigoma.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mapema leo, Matola amesema kuwa unapocheza na timu kama Tabora United inakua ni mechi nguma kwani wamewaangalia mechi nyingi na kusisitiza kuwa hautakua mchezo mrahisi lakini wamejiandaa vizuri kupata alama tatu kwenye mchezo huo.

“Tupo vizuri pamoja na ugumu wao lakini tumejiandaa  kuhakikisha tunapata matokeo ya pointi tatu kwenye mchezo wa kesho  kwani ni muhimu.” Amesema kocha huyo.

Aidha katika hatua nyingine Matola amesema kuwa licha ya ugumu wa ratiba uliopo lakini wamejipanga vyema kwani wana kikosi kikubwa na wapo tayari kwa michezo yote iliyopo mbele yao.

Katika mchezo wa kesho utakaochezwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora, saa 10:00 alasiri, Simba wanashuka dimbani  wakiwa nafasi ya 3 wakifanikiwa kuvuna pointi 26 katika michezo 11 huku Tabora United wakishuka dimbani mara 13 wakivuna pointi 15, nafasi ya 12 katika msimamo.

Habari Zifananazo

Back to top button