Matukio 10 ya kukumbukwa mwaka 2022

Matukio 10 ya kukumbukwa mwaka 2022

MWAKA 2022 unamalizika leo Jumamosi Desemba 31, tunaukaribisha mwaka mpya wa 2023.

Mwaka 2022 kila mmoja anaweza akaulelezea kwa namna yake, kwani yapo matukio yaliyoleta furaha, lakini pia yapo yaliyoacha majonzi.

Yafuatayo ni matukoo 10 ya kukumbukwa mwaka 2022.

Advertisement

Ndugai ajiuzulu Uspika

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, alijiuzulu wadhifa wake siku ya Alhamisi Januari 6, 2022.

Kwa mujibu wa barua aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.

“Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo tarehe 06 Januari 2022, nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa bunge la Jamhuri ..

” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Job Ndugai.

Dk Tulia Ackson Spika mpya

Kufuatia kujiuzulu kwa Job Ndugai kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Mbunge wa Mbeya Mjini, ambaye pia alikuwa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alishinda nafasi ya uspika katika uchaguzi uliofanyika Februari 1 na kupata kura zote 376 za wabunge waliohudhuria uchaguzi uliofanyika, bungeni jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson

Mbowe atoka gerezani

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe aliachiliwa huru, baada ya kukaa mahabusu kwa siku 216  tangu alipokamatwa Julai 21, 2021 kwa tuhuma kadhaa ikiwemo ya kula njama, kupanga na  kufadhili ugaidi.

Saa chache mara baada ya Mbowe kuachiwa alialikwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo alinukuliwa akisema miongoni mwa waliyozungumza ni pamoja na kuwa na maridhiano.

Polepole ateuliwa Balozi Malawi

Machi 14, 2022 Hamphrey Polepole aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, aliteuliwa kuwa balozi na Machi 15 aliapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Balozi Polepole.

Rais Samia azindua Filamu ya Royal Tour

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alizindua  filamu ya Tanzania The Royal Tour katika ukumbi wa Guggenheim Museum, New York nchini Marekani, Aprili 21, 2022

Katika uzinduzi huo Rais Samia alipata wasaa wa kuzungumzia  fursa zilizopo Tanzania, vivutio  na kuwaasa raia wa Marekani na dunia kwa ujumla kuja Tanzania kufanya utalii na kuwekeza.

Moja ya jambo ambalo liliwavutia wengi ni pale Rais Samia alipotanabaisha kuwa kitendo cha yeye kuendesha gari kwenye utengenezaji wa filamu hiyo, ilikuwa ni cha mara kwanza baada ya miaka 15.

Filamu ya The Royal Tour.

Sensa ya Watu na makazi

Rais Samia Suluhu Hassan alizindua  matokeo ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi na kutangaza kuwa Tanzania ina jumla ya watu 61,741120.

Rais Samia alitangaza  idadi hiyo katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo alisema kuwa kati yaiIdadi hiyo ya watu, Tanzania Bara ina  watu 59,851,357 na Zanzibar ni watu 1,889,773.

Amefafanua kuwa kati ya idadi hiyo wanawake ni 31,688,790 sawa na asilimia 51 na wanaume ni 30,53130 sawa na asilimia 49.

Alieleza kuwa idadi hiyo ni ongezeko la watu zaidi ya milioni 19 ukilinganisha na sensa ya miaka kumi iliyopita, yaani mwaka 2012 ambapo kipindi hicho idadi ilikuwa 44,928923.

Ndege ya Precision yaanguka:

Novembea 6, 2022 ilikuwa siku ya vilio na huzuni kufuatia kuanguka kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Precision Air, ambayo iliangukia katika Ziwa Victoria karibu na Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera. Katika ajali hiyo abiria  19 walipoteza maisha.

Ndege ya Precision Air iliyopata ajali.

Shujaa Majaliwa apelekwa jeshi, atinga bungeni

Novemba 8, 2022, mvuvi  shujaa aliyekuwa sehemu ya kikosi cha watu waliookoa maisha ya abiria 24 walionusurika kwenye ajali ya ndege ya shirika la Precision, Majaliwa Jackson alitunukiwa kazi kwenye kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania.

Rais, Samia Suluhu Hassan, alitoa amri hiyo siku ya  Jumatatu, Novemba 7, 2022, kwamba Majaliwa apewe mafunzo na ajira katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na alizawadiwa Sh milioni  4.3

November 11, 2022, Majaliwa alipokelewa bungeni na Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson alitangaza  kuwa wabunge wamechanga kiasi cha Sh 5,023,000 kwa lengo la kumpongeza kijana huyo.

Kijana Majaliwa (wa Kwanza Kulia) akiwa bungeni.

Rais Samia  awasili Washigton Dc

Desemba 14, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki mkutano wa viongozi wa Afrika na Marekani uliofanyika kwa siku tatu jijini Washington DC nchini Marekani.

Hiyo ilikuwa  safari yake ya pili nchini humo kwa mwaka 2022, baada ya ile ya uzinduzi wa filamu ya ‘The Royal Tour’.

Rais Samia amefanya ziara za mara kwa mara nje ya nchi, jambo linalotajwa kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na jumuiya za kimataifa.

Bwala la Nyerere kujazwa Maji 

Desemba 22, 2022 Tanzania, Afrika na dunia kwa ujumla ilishuhudia Rais Samia akizindua shughuli ya kujaza maji katika Bwawa la Mradi wa Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) katika Mto Rufiji.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *