Matumizi ya akili bandia kurahisisha matibabu

MATUMIZI ya akili bandia katika sekta ya afya yatamwezesha mgonjwa kugundua mapema magonjwa yanayomsumbua ili waweze kupata matibabu ndani ya muda mfupi.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili katika Hospitali ya Taifa Afya ya Akili ya Mirembe iliyopo jijini Dodoma, Innocent Mwombeki amesema hayo.

“Katika sekta ya afya kuna changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa wataalam, ukosekanaji wa teknolojia katika huduma za afya hali inayosababisha watu wanashindwa kugundua magonjwa yao mapema na matokeo wanaweza kuingia kwenye hali mbaya ya ugonjwa.

Advertisement

“Hali hiyo inasababisha vifo au ulemavu hivyo kuwa mzigo kwa taifa,” amesema.

Amesema kupitia mradi wa kuboresha huduma ya afya ya akili pamoja na mradi wa magonjwa ya moyo ambayo itahusisha utumiaji wa akili bandia utawezesha watanzania kutambua afya zao mapema na watoa huduma kufanya uamuzi kwa urahisi kutatua changamoto inayomkabili mgonjwa.

Amesema lengo ni kuwezesha matibabu yapatikane kwa muda mfupi.

Mwombeki ni miongoni mwa watafiti saba waliopewa fedha za kuwezesha utafiti wanaoufanya na serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo alisema sh bilioni 1.

29 zitatumika katika utekelezaji wa miradi saba ya wabunifu kutoka taasisi mbalimbali nchini.

Profesa Nombo alisema fedha hizo zinatokana na tengeo katika bajeti kuu ya serikali pamoja na michango ya washirika wa maendeleo hususan Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Utafiti la Canada (IDRC) na Shirika la Maendeleo la Taifa la Norway (NORAD).

8 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *