Matumla ampa kiburi Njopeka, atamba kumchapa Kitogo

DAR ES SALAAM: Bondia Jumanne Njopeka wa Kawe Ukwamani ameweka kambi kwa mkongwe Rashid Matumla ili kumlambisha sakafu Bakari Kitogo wa Temeke Katika pambano la safari ya Beach, Oktoba 22 mwaka huu.
Pambano hilo litafanyika katika viwanja vya fukwe ya Rongoni Kigamboni Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa mazoezi akiwa kambini kwa mkongwe Matumla Mbagala Dar es Salaam Njopeka amesema anafanya mazoezi kiroho mbaya.
“Nafanya mazoezi kiroho Mbaya kuhakikisha mpinzani wangu anapokea kichapo cha aina yake katika pambano letu ajipange.”amesema Njopeka
Kwa upande wake kocha wa Bondia huyo Rashid Matumla amesema kutakuwa na mapambano ya kuvutia siku hiyo kutokana na jinsi mabondia wanavyojiandaa.
“Mabondia wote wamejiandaa na wapo vizuri kwa pambano mashabiki wajitokeze kwa wingi.”amesema Matumla.