Mauaji Njombe yaacha maswali, Polisi wajitosa

NJOMBE: Wananchi wa Iwawa wilayani Makete Mkoa wa Njombe wametakiwa kuacha kufanya matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakileta taharuki kwa jamii kwa kuamini Imani za kishirikina.

Akizungumza leo Januari 11, 2024 Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Mahamoud Hassan Banga wakati akitoa pole kwa wafiwa ambao ndugu yao aliuawa kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili, amesema jamii itaendelea kupewa elimu ili kuweza kuondokana na imani potofu ambazo zimekuwa zikileta mauaji na kuzua taharuki.

Pia, amewataka wananchi na ndugu kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa wa tukio hilo kwa mujibu wa sheria ili kutokomeza matukio kama hayo katika jamii.

Vilevile, amewaasa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo mara nyingi vimekuwa vikitokea lakini baadhi wamekuwa wakificha bila kutoa taarifa sehemu sahihi hivyo waendelee kushirikiana kwa pamoja na jeshi la polisi kutokomeza vitendo hivyo.

Habari Zifananazo

Back to top button