Mauki ataja dalili za ugonjwa wa afya ya akili

Kati ya watu wanne mmoja anachangamoto ya afya ya akili

DAR ES SALAAM: MTAALAM wa Saikolojia Dk Chris Mauki ameeleza dalili za afya akili nchini kuwa ni pamoja na kukosa usingizi vizuri kunakosababisha wengine kuchukua hatua za kunywa kilevi, kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na wanaume pia.

Dalili nyingine ni kuongezeka uzito wa ghafla wakati vyakula havijabadilika, hasira za mara Kwa mara, magonjwa ya vidonda vya tumboni,ngozi, ini na hata magonjwa ya moyo.

Dk Mauki ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Da er Salaam (UDSM) amesema hayo leo Dar es Salaam katika kilele cha waajiri bonanza lililoandaliwa na Chama Cha Waajiri nchini (ATE) likiambatana na michezo mbalimbali pamoja na kupima afya,Kauli mbiu ikiwa ni kuimarisha afya ya akili Ili kuongeza tija mahala pa kazi.

Akizungumza katika bonanza hilo, Dk Mauki amesema wengi wamekuwa wakitafsiri vibaya tatizo la afya ya akili kuwa ni wale wanaopelekwa hospitali ya vichaa Mirembe pekee ndio walengwa wa tatizo la afya ya akili.

“Wengi wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali kazini na hata nyumbani…pale unapojiona hauko sawa ni vyema kufahamu ndipo changamoto ya afya ya akili huanzia,” amesema Dk Mauki na kuongeza kuwa changamoto ya afya ya akili ni vitu vidogovidogo vinavyoweza kuzuilika na ukiona aliyefikia hatua ya matibabu alishindwa kuhimili.

Amesema wapo wanaokosa hamu ya tendo la ndoa huku wakioona wenza wao ndio wenye shida na hata kufikia kuwaita ”mbwa’ ijulikane kuwa hapo ndipo afya ya akili huanzia hivyo hatua zichukuliwe kwa kuwashauri na kutowanyanyapaa walengwa.

“Jitahidini kushughulikia matatizo ya ndoa,wataalam wanasema moyo una nafasi ya asilimia 60 ya mahusiano..ambapo wapo wenye magari na fedha lakini wakajikuta wakishindwa kwenda kazini kutokana na mahusiano mabaya.

Aidha amesema tafiti za mwaka Jana 2022 zinaeleza kuwa kati ya watu wanne mmoja wao ana changamoto ya afya ya akili,na Kila sekunde 40 watu watatu hujiua wenyewe duniani.

Dk Mauki amesema ipo haja Kwa kampuni au taasisi mbalimbali kusaidia watu wao kuwa na mazingira salama ya kazi kuwawekea mifumo ya mazoezi ya mwili na michezo na kwamba bila hivyo watu wataendelea kupotea.

Mtendaji Mkuu wa ATE,Suzanne Ndomba-Doran amesema mazoezi sehemu za kazi husaidia kuwa na utulivu na kuwa na matokeo chanya.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work At Home
Work At Home
1 month ago

Earn money in USA, high scores from trusted resources. Work at your own pace. Regular Payments. Search in different job categories. Work anywhere on your vs03 computer, laptop or mobile phone. Update your profile at any time.
.
.
Detail Here———->>> http://Www.Smartcash1.com

KariTeter
KariTeter
1 month ago

Single Mom With 4 Kids Lost Her Job But Was Able To Stay On Top By Banking Continuously DOLLER 1500 Per Week With An Online Work She Found Over The Internet… 

Check The Details HERE…..  https://careerstars12.blogspot.com/

Last edited 1 month ago by KariTeter
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x