Mavunde achangia ujenzi wa shule

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde leo Desemba 2,2023 amekabidhi mifuko 500 ya saruji kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma John Kayombo.

Lengo la kutoa saruji hiyo ni kuchochea ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo kwa shule za Msingi na Sekondari Dodoma Jiji.

Akizungumza wakati wa kukabidhi saruji hiyo Mavunde amesema katika mwaka huu wa fedha miradi mingi mikubwa ya ujenzi wa shule mpya za msingi na aekondari inatekelezwa ndani ya kipindi kifupi.

“Katika kuunga mkono jitihada za serikali,mimi pamoja na wananchi tumekuwa tukianzisha ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu jijini Dodoma, “amesema na kuongeza

” Katika kuendelea kuchochea shughuli za maendeleo kwenye sekta ya elimu nimechangia mifuko 500 ya saruji ili iendeleze ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika maeneo mbalimbali ya Dodoma jiji,”amesisitiza

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma John Kayombo amemshukuru Mavunde kwa mchango wa saruji wenye thamani ya sh milioni 9 na kwa kuwa mstari wa mbele katika shughuli za maendeleo na hasa sekta ya elimu na kuahidi kuisimamia mifuko hiyo ili ifanye kazi iliyokusudiwa ya ujenzi wa madarasa.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button