Mavunde akabidhi mtambo wa Sola

Wasimikwa wadi ya mama na mtoto

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amekabidhi mtambo wa kuzalisha umeme jua ‘Sun King Inverter wa 5.1kv’
Mtambo huo una  thamani ya  sh milioni 7 ,  umesimikwa kwenye jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mtambo huo, Mavunde aliishukuru Kampuni ya Sun King kwa kuunga mkono jitihada za  Rais Dkt. Samia Suluhu  Hassan za kuboresha huduma za Afya nchini na hususani huduma inayomlenga mama na mtoto katika mkoa wa Dodoma.
Amesema, mtambo huo Mtambo huo utasaidia kuhakikisha huduma ya nishati ya umeme inapatikana muda wote katika jengo hilo la huduma ya mama na mtoto.
“Tutaendelea  kuthamini mchango mkubwa ambao unaofanywa na kampuni binafsi ambazo zimekua zikiwekeza  kwa ajili ya kuhudumia jamii kama vile kwenye vituo vya afya,  shule,   sekta ya kilimo na nyinginezo.
Naye Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Sun King Tanzania , Juma Mohamed amesema kampuni yao imejipanga vyema kusaidiana na wadau mbalimbali katika kuboresha huduma za Msingi za Jamii ikiwemo Afya na Elimu kupitia bidhaa mbalimbali wanazozalisha na pia ametoa fursa ya ajira kwa vijana kama mawakala wa bidhaa za sola.
Akitoa shukrani kwa niaba,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa Mkoa wa Dodoma Dkt. Peter Mbele amemshukuru Mavunde kwa kuwa bega kwa bega na uongozi wa Hospital katika kuboresha huduma za Afya..

Habari Zifananazo

Back to top button