Mavunde akabidhi viti mwendo SHIVYWATA

MBUNGE wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amekabidhi vitu mwendo ,wheelchair’ vyenye thamani ya Sh milioni 4 kwa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu mkoani Dodoma (SHIVYWATA).

Lengo la kukabidhi viti mwendo hivyo ni kuelekekea katika kilele cha siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu.

Mavunde ametumia fursa hiyo pia kujadiliana na uongozi wa Shirikisho juu ya maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu kwa kugharamia sehemu ya maandalizi ya kuwasafirisha wajumbe.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa SHIVYWATA-DODOMA Omary Lubuva amemshukuru Mavunde ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho hilo Dodoma kwa kuwa karibu nao siku zote na kwa msaada mkubwa wa mara kwa mara wa viti mwendo ambao amekuwa akitoa kwa watu wenye uhitaji mkoani Dodoma

Habari Zifananazo

Back to top button