Mavunde akikubali chuo cha ujuzi Kahama

WAZIRI wa Madini nchini Anthony Mavunde amesema uwekezaji wa chuo cha Mafunzo ya Ubunifu, Maarifa na Ujuzi kilichoanzishwa Buzwagi Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kimechukua mafomeni na warakibu zaidi ya 2000 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa mwaka 2024.

Kituo hicho pia kinatoa mafunzo ya maamuzi, usuluhushi wa migogoro na uendeshaji wa usimamizi wa gharama katika sekta ya madini.

Waziri Mavunde amesema hayo leo alipokuwa akifungua rasmi chuo hicho kinachosimamiwa na Kampuni ya Dhahabu ya Barrick huku akieleza kuwepo kwa chuo hicho kutaipunguzia Serikali gharama ya kuwapeleka wataalamu nje ya nchi kwenda kujifunza.

“Serikali tunayo mikakati ya kuendelea kunufaisha wananchi wetu nakutaka vijana wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa na eneo hili lina ukubwa wa ekari 1333 na limepewa leseni maalum kuwa ukanda wa kiuchumi yaani Buzwagi (Economic Zone)”amesema Mavunde.

Mavunde amesema eneo hili litakuwa na viwanda zaidi 100 litatoa mchango mkubwa nakuwa sehemu ya kufanya tathimini ya madini hapa na Serikali itanufaika kupitia kodi,ushuru na huduma za miradi ya jamii.

Ofisa mkuu wa uendeshaji wa Barrick Ukanda wa Afrika Mashariki ya kati Sebastian Bock alisema Uwanja wa ndege na chuo ni sehemu ya mpango ya kuibadilisha Buzwagi kuwa ukanda maalum wa kiuchumi.

“Upembuzi yakinifu uliofanyika mwaka 2021 uliionyesha kuwa uundawaji wa Kanda Maalum kiuchumi ukiwa na uwezo wa kuchukua nafasi ya Mgodi huo Kama kichochoe Cha uchumi wa eneo na kutoa ajira 3000 kila mwaka”amesema Bock.

Mbunge wa jimbo la Kahama Jumanne Kishimba amesema kampuni ya Barrick imekuwa ya kwanza kuwekeza katika eneo hili kwenye sekta ya elimu hivyo aliomba wachombaji wadogo wapatiwe.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama amesema Barrick wameonesha muungano kwa kampuni ya Twiga ya Tanzania kuwajali Watanzania kuwekeza elimu kwani wanajifunza mambo ya madini ikiwa Kahama ina eneo kubwa la uchimbaji hata kwenye ilani suala hilo lipo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita amesema Barrick wamekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia sekta ya elimu na afya na kuisaidia shughuliza za ujasiriamali kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu.

Habari Zifananazo

Back to top button