Mavunde atunukiwa tuzo ya shukrani

NAIBU Waziri wa Kilimo ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde ametunukiwa tuzo ya shukrani na jukwaa la Wajasiriamali mkoani Dodoma .

Tuzo hiyo ni ya kutambua mchango wa Mavunde katika kuwawezesha wakinamama kiuchumi kupitia program mbali mbali alizozianzisha ndani ya mkoa huo.

Tuzo hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule kwa niaba ya wanajukwaa wakati wa kongamano kubwa la Wajasiriamali wakina mama wa mkoa wa Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa kanisa katoliki la Mt Paulo Msalaba.

Awali Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Maryrobbi Mabhaya amesema tuzo hiyo imetolewa maalum kwa ajili ya kuthamini na kuenzi mchango mkubwa wa mbunge huyo kwa maendeleo ya wakina mama Dodoma na hasa katika kuwatafutia fursa na uwezeshwaji kiuchumi.

Aidha, Senyamule amewataka wakina Mama wa Dodoma kuchangamkia fursa zaidi zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan hasa katika eneo la kilimo cha mashamba makubwa ya pamoja ya ‘block farms.

Ne Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewashukuru wakina mama wa Dodoma kwa kutambua mchango wake katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi ya wakina mama Dodoma na kuahidi kuja na programu mbalimbali nyingi zaidi za kuwajengea uwezo na kuwawezesha ikiwemo hatua ya sasa ya kutafuta Taasisi ya fedha ambayo itawakopesha wakina mama wajane bila riba.

Habari Zifananazo

Back to top button