MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amekabidhi tofali ndogo 10,000 kwa uongozi wa Soko la Mavunde Chang’ombe,Jijini Dodoma.
Lengo la kutoa tofali hizo ni kuboresha mandhari ya soko hilo na miundombinu yake.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye soko hilo,lililojengwa kwa pamoja kati ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mbunge Mavunde,wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero na changamoto za wafanyabiashara hao.
“Mtakumbuka wakati wa uchaguzi niliahidi kuboresha soko letu ili kuwa na mandhari rafiki na kupunguza vumbi ambalo lina athari kwa bidhaa mnazouza.”Amesema Mavunde na kuongeza
” Leo nina furaha kuja hapa kutimiza ahadi yangu ya kuboresha mandhari ya soko letu kwa kukabidhi paving blocks hizi 10,000 ambazo zitasaidia kubadlisha muonekano wa soko letu katika eneo la mbele la mapokezi.”Amesema
Gharama za matengenezo ya soko Hilo ni sh milioni 10 ili kulipa muonekano mpya.
“Nitaendelea kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha mazingira mazuri biashara kwa wafanyabiashara wadogo na hasa katika kuwaweka kwenye mazingira rafiki ya kufanya biashara.” Amesema Mavunde
Nae, Diwani wa Kata ya Chang’ombe Bakari Fundikira, amemshukuru Mavunde kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa soko hilo na ambavyo anaendelea kulihudumia siku hadi siku.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Soko Hilo, Menas Mlelwa ameshukuru kazi kubwa inayofanyika ya kuboresha soko hilo na kutumia fursa hiyo kushukuru ahadi ya Mbunge ya Tanki la Maji la Lita 5000 pamoja na TV kubwa mbili kwa ajili ya soko.
Mwandishi WetuAugust 26, 2023