WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana amemteua Alli Mayay Tembele kuwa mwakilishi wa Tanzania Katika Bodi ya Ushauri wa Michezo ya Jumuiya ya Madola (CABOS) kwa miaka mitatu.
Taarifa iliyotolewa leo Machi 10, 2023 na Kitengo cha Mawasiliano kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, imeeleza kuwa hatua hiyo imetokana na Tanzania kuimarika kidiplomasia katika nyanja za michezo.
Alli Mayay ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini na sasa ataiwakilisha nchi katika Bodi ya CABOS na kuwa mjumbe mwakilishi wa Bara la Afrika.
CABOS ni Chombo cha kumshauri Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na serikali wanachama kuhakikisha kunakuwa na ushirikishwaji thabiti wa serikali na uwakilishi katika maendeleo ya sera ma utekezaji wake.