Mayele aomba kura Watanzania uchezaji bora DRC

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele amewaomba wadau wa soka nchini kumpigia kura, ili aweze kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka nchini kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Kupitia akaunti yake ya Instagra, Mayele amewaomba mashabiki wa soka nchini kumpigia kura, ili aweze kushinda tuzo hiyo, ambayo inawaniwa na wachezaji saba wanaocheza soka kwenye mataifa mbalimbali ya Afrika na Ulaya.

“Nimebahatika kuingia kwenye kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2022, nawaomba wananchi kunipigia kura, ili niweze kushinda tuzo hiyo,” amesema Mayele.

Mshambuliaji huyo ameingia kwenye kinyang’anyiro baada ya kufanya vizuri kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akimaliza nafasi ya pili katika mbio za ufungaji bora akifunga mabao 16 nyuma ya George Mpole na msimu huu mpaka sasa anaongoza kwenye mbio za ufungaji bora akifunga mabao 11.-

“Nimebahatika kuingia kwenye kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2022, nawaomba wananchi kunipigia kura, ili niweze kushinda tuzo hiyo,” amesema Mayele.

Wachezaji wengine anaoshindana nao kuwania tuzo hiyo. Huku majina ya timu nan chi kwenye mabano ni Neeskens Kebano (Fulham, England), Jackson Muleka (Beşiktaş, Uturuki) na Chancel  Mbemba (Marseille, Ufaransa).

Wengine ni Yoane Wissa (Brentford, England), Dieumerci  Mbokani (S.K Beveren, Ubelgiji) na Meshack Elia (TP Mazembe, DRC).

Habari Zifananazo

Back to top button