Mayele awashukuru Yanga kumuamini

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele ameushukuru uongozi wa timu hiyo pamoja na benchi la ufundi kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kudhihirisha kipaji alichokuwa nacho.

Akizungumza na HabariLeo, kinara huyo wa mabao wa Yanga, alisema mafanikio aliyokuwa nayo hivi sasa yanatokana na imani ya pande hizo mbili na siku zote ataendelea kuziheshimu.

“Juzi nimeitwa timu ya taifa ya DR Congo, ni kutokana na kiwango bora nikiwa na timu yangu ya Yanga, naushukuru uongozi, benchi la ufundi na wachezaji wenzangu kwa kunipa ushirikiano tangu nije hapa,” amesema Mayele.

Mshambuliaji huyo ameeleza kuwa kwa sasa ataendelea kupambana kuipigania timu yake kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara,  na tuzo ya mfungaji bora ambayo kwa sasa yeye ndio kinara akifunga mabao 15.

Habari Zifananazo

Back to top button