BAADA ya kuibuka sintofahamu kuhusu aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kutokana na ujumbe wake kwenye mtandao wa Instagram, nyota huyo raia wa DR Congo amesema ataweka wazi kila kitu kinachoendelea.
Saa 12 zilizopita Mayele aliandika “Chuki ya nini mimi sio Mtanzania bhona nilikosea kucheza timu za Tanzania ni nini”.
Baada ya kuandika jumbe hiyo yenye maoni zaidi ya 8,000, Mayele ameibuka tena saa mbili zilizopita na kuandika: Jioni nitakuwa na live nitaongea kila kitu simuogopi mtu naogopa Mungu Wallah”.
Watu mbalimbali akiwemo Haji Manara wametoa maoni yao kuhusu jumbe hiyo ambapo amemtaka mchezaji huyo kufuta jumbe hiyo. “My brother please futa hii sio nzuri”.