Mayele rasmi Pyramids

KLABU ya Pyramids imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji, Fiston Mayele kutoka Young Africans.

Mayele alisajiliwa na Yanga mwaka 2021 akitokea AS Vita ambako alikuwa mshambuliaji wa pili kinara wa ufungaji katika ligi ya nchini DR Congo akipachika mabao 13 akizidiwa bao moja pekee na Jean Baleke aliyekuwa TP Mazembe.

Akiwa na Yanga kwa misimu miwili, Mayele ameisaidia kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu mara 2, Kombe la FA mara 2 na Ngao ya Jamii mara 2 na kuifikisha Yanga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mayele amepewa jezi namba 9 katika klabu yake mpya, namba ambayo alivaa akiwa na Yanga.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button