CHAMA cha kiongozi wa upinzani wa Senegal aliyefungwa jela, Ousmane Sonko kimesema kitamteua mgombea mbadala wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa 2024.
–
Hatua hiyo ni baada ya mahakama nchini humo kutoa uamuzi kuwa kiongozi huyo hatoweza kuwania urais katika uchaguzi ujao.
–
Chama cha Afrika cha Senegal, Kazi Maadili na Udugu (PASTEF) kimempendekeza Katibu Mkuu wake, Bassirou Diomaye Faye kupeperusha bendera ya chama hicho.
–
“Kumfadhili mgombea Bassirou Diomaye Faye hakumaanishi kwa vyovyote vile kumsaliti ugombea wa Ousmane Sonko.” Taarifa ya chama alisema.


Add a comment