Mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe amesema “hatapoteza nguvu zake kwa mambo yasiyo na maana” alipoulizwa kuhusu kejeli za mlinda mlango wa Argentina Emiliano Martinez baada ya fainali ya Kombe la Dunia.
“Sherehe sio shida yangu,” Mbappe aliambia RMC Sport.”Sipotezi nguvu kwa mambo kama haya yasiyo na maana.”amesema Mbappe.
Hatua hiyo ni baada ya Martinez kubeba kinyago cha Mbappe huko Argentina ambako walikuwa wakisherehekea ubingwa wa mashindano ya Kombe la Dunia.
Martinez alionesha ishara mbaya baada ya kutwaa kombe la dunia na kuwa kipa bora wa michuano hiyo baada ya ushindi wa mikwaju ya penalti kwa Argentina mnamo Disemba 18.