Mbappe sasa mfungaji bora PSG

BAADA ya kufunga bao moja katika mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Nantes jana, Kylian Mbappe amekuwa mfungaji bora wa muda wote wa Paris Saint Germain (PSG).

Mbappe aliifungia bao hilo dakika ya 92+ katika ushindi wa mabao 4-2na kufikisha mabao 201 na kuvunja rekodi ya Edison Cavani, aliyekuwa akishirikia rekodi hiyo kwa kuwa na mabao 200.

Mshambuliaji huyo wa Ufaransa, ambaye alitimiza umri wa miaka 24 mwezi Desemba, ameendelea kuthibitisha ubora wake kwa kuweka rekodi mbalimbali ikiwemo mchezaji mwenye umri mdogo 22, kufikisha mabao 100 akiwazidi Messi na Ronaldo ambao hawakuwahi kufunga idadi hiyo wakiwa na umri huo.

“Ninacheza kuweka historia,” alisema Mbappe, ambaye alijiunga mwaka wa 2017 kwa mkopo kutoka Monaco kabla ya uhamisho wa euro 180m.

Katika orodha ya wafungaji wa PSG wa muda wote, namba tatu anashikilia Zlatan Ibrahimovic ambaye ana mabao 156 akifuatiwa na Neymar 118.

Habari Zifananazo

Back to top button