Mbaroni akidaiwa kukutwa na meno ya tembo Arusha

Mbaroni akidaiwa kukutwa na meno ya tembo Arusha

POLISI mkoani Arusha inamshikilia Reginald Ambros (42) maarufu kama Amsi kwa kukutwa na vipande viwili vya meno ya tembo.

Taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Justine Masejo, amesema mkulima huyo alikutwa na vipande hivyo, akiwa amevifunga ndani ya boksi

“Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na matukio ya biashara haramu ya uuzaji wa nyara za serikali, ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji, ili kupata mtandao mzima,” alisema Kamishna huyo.

Advertisement

Pia alisema jeshi hilo lilifanikiwa kukamata jumla ya lita 1,480 za pombe haramu aina ya gongo, mitambo 80 ya kutengeneza pombe hiyo pamoja na watuhumiwa 62, ambao wamefikishwa mhakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.