MOROGORO; JESHI la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia Roda Peter (30) mkazi wa Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma ya kuua watoto wawili wachanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema mtuhumiwa ambaye ni mkulima na mkazi wa Kata ya Kihonda, anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 12, 2023, maeneo ya Kihonda kwa kuwaweka kwenye mifuko miwili tofauti ya safleti, kisha kuwatupa kichakani.
“Siku za hivi karibuni kuna mmama alijifungua na kutupa watoto wake wachanga ambao ni mapacha …sasa katika upelelezi wetu kwa kushirikiana na wananchi tulifanya ufuatiliaji na kumbaini huyo mama tumefanikiwa kumkamata anaitwa Roda Peter, “ alisema Mkama.
Amesema upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.