Mbegu za asili fiwi, ulezi hatarini kutoweka

MBEGU za asili za fiwi, ulezi , njugu mawe zipo hatarini kutoweka, katika mikoa ya Kanda ya Kusini.

Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Kanda Kusini (Tari), Naliendele Dk. John Tenga, amesema hayo akizungumza na HabariLEO kwenye viwanja vya Nanenane vya Ngongo mjini Lindi, amesema kwamba mbegu hizo kwa sasa zinatoweka.

Amesema kuwa jitihada inafanywa kwa kituo kufanya utafiti kuhakikisha mbegu zote za asili zinarudi tena kwa kushirikiana na wakulima na kuziboresha,ili kuzalisha mazao kwa wingi.

Advertisement

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa shirika la Sswisaid, Betty Malaki amesema kuwa shirika hilo linafanya jitihada kwa kushirikiana na wadau mbegu za asili zitumike kuzalisha mazao na kuliwa chakula cha asili na kuondokana na kutumia mbegu za nje.

Amesema mpaka sasa wakulima wa Kanda ya Kusini walishapewa elimu na kubadilishana mbegu za asili, na sanjari kufungua benki ya mbegu za asili.

5 comments

Comments are closed.