Mbinu zinazoweza kutumika kuwaleta kwa wingi watalii
TANZANIA imejaliwa kuwa na maeneo mengi ya maliasili zikiwemo hifadhi za wanyamapori, misitu na malikale ambayo yana mchango mkubwa kwa mazingira, wananchi na ukuaji wa uchumiwa taifa. Yapo maeneo yenye kutoa maji kwa matumizi mbalimbali, makazi ya wanyamapori na viumbe wengine, uchavushaji, uhifadhi wa udongo, ufyonzaji wa hewa ukaa (carbon) inayopunguza kutokea athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kiuchumi, maliasili na malikale zimeendelea kuchangia kwa kiwango kikubwa fedha za kigeni na Pato la Taifa (GDP) kupitia utalii, ajira, nishati, elimu, utafiti, utamaduni,burudani na tiba.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopo kwenye tovuti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, sekta ya utalii huchangia takribani asilimia 25 ya fedha za kigeni na zaidi ya asilimia 17 katika Pato la Taifa. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa baada ya kupokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake, Dk Pindi Chana, yeye ameona kwamba mchango wa pato la taifa kwa asilimia hizo linalotokana nawizara yenye kusimamia rasilimali za asili nyingi, halitoshi.
Kutokutosha huko kunatokana naukweli kwamba Tanzania ina rasilimalinyingi za maliasili na vivituovingi vya utalii ikilinganishwa na baadhi ya nchi nyingine.Anasema pamoja na kazi nzuri za uhifadhi zinazofanywa na Tawa na taasisi zingine za uhifadhi, bado mchango kwa pato la taifa kutoka kwa sekta za wizara hiyo ni mdogo.
“Watanzania wana matumaini makubwa nasi na wizara hii mchango wake katika pato la taifa linafikia asilimia 21 hadi 25, lakini haitoshi kwa taifa lililosheheni kilakitu,” anasema Mchengerwa.
Mchengerwa anabainisha haya siku moja baada ya kuapishwa kwake kuongoza wizara hiyo na kuanza kazi kwenye ziara ya kwanza katika makao makuu ya Tawa yaliyopo mkoani Morogoro. Anasema wanayo kazi kubwa ya kufanya katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa na kwa kufanikisha hilo na aliwataka watendaji wa taasisi zilizopo chini ya wizara kuwasilisha taarifa kwake haraka.
Mchengerwa anasema lengo ni kuona namna ya kupanga mikakati ya kuongeza idadi ya watalii
watakaochangia kuongezeka kwa asilimia ya mchango wa wizara kwa Pato la Taifa kupitia sekta ya utalii na masuala mengine ya kimenejimenti. “Kwa sasa kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuongeza angalau mchango wa wizara kwenye Pato la Taifa ufikie angalau asilimia 33,”anasema Mchengerwa.
Anawaagiza watumishi wa wizarahiyo kujipanga katika kuhifadhi rasilimali za taifa, kuongeza kasi ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kufanya kazi kwa bidii.
“Nitataka kila mmoja wetu akafanye kazi kwenye eneo lake na afanye kazi kwelikweli, kama utatakiwa kuwepo kwenye eneo lako saa sita mchana uwepo kwenye eneo lako,” anasisitiza Mchengerwa.
Anataka pia vivutio vyote katika kila mkoa vijulikane, kutambuliwa na kutangazwa kwa ajili ya kuongeza utalii wa ndani na wa wa nje.
Anasema Royal Tour ni moja ya jitihada za kimkakati ya Awamu ya Sita zilizolenga kuvutia watalii na uwekezaji nchini na kwamba filamu hiyo imeshaanza kuleta matokeo chanya katika sekta ya utalii. “Rais wetu ametoka kufanya filamu ya Royal Tour, katuanzishia