Korosho Marathon zahitimishwa leo Mtwara

MSIMU wa pili wa mbio za Krosho Marathon 2023, umekamilika leo katika viwanda vya Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Mbio hizo zimeandaliwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) na zilikuwa na umbali wa kilomita 21 ambayo mshindi wa kwanza amepatiwa Sh milioni 4, wa mwisho katika mbio hizo Sh laki 4, pia kilomita 10 ambayo mshindi wa kwanza alipatiwa Sh milioni 2.5 wa mwisho Sh 50,000.

Mshindi wa kwanza mwanaume mbio za kilometa 21 Faraja Lazaro kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amejipatia kitita cha Sh milioni 4, amesema ushindi huo umetokanana na mazoezi tu na siyo vinginevyo hivyo amewashukuru waandaji wa mbio hizo na serikali kwa ujumla kwa jitihada kubwa za kufanikisha jambo hilo’’

‘’Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia hii nafasi kwani wengi walitamani kufikia nafasi hii na tulikuwa wengi tuliyokimbia ila mimi Mwenyezi Mungu amenipa hii nafasi pia niwashukuru sana waliyoandaa haya mashindano, ni mazuri’’amesema Lazaro

Mshindi mwingine wa kwanza ambaye ni mwanamke katika kilometa hizo za kometa 21, Failuna Mtanga kutoka mkoani Arusha naye pia amejinyakulia kitita ya Sh milioni 4.

“Fedha hizi nilizopata nitaenda kufanya matumizi ya kawaida tu na nawashauri wanawake wenzangu nawafanye mazoezi ya mara kwa mara na waweze kushiriki mbio kama hizi na zingine”amesema

Mkurugenzi Mkuu wa Cbt, Francis Alfred amesema mbio hizo kwa mwaka huu 2023 zimekuwa tofauti na ya mwaka 2022 kutokana na maandalizi, ushiriki wa wadau wote katika kulifanikisha jambo hilo umekuwa mzuri.

Mgeni rasmi katika kilele cha mbio hizo ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button