Mbogamboga, matunda chanzo cha kipindupindu

DODOMA: Watafiti wametaja kuwa ulaji wa mboga mboga na matunda umekuwa chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu, huku wanawake wakionekana kuathiriwa zaidi na ugonjwa huo wa mlipuko.

Mhadhiri Msaidizi na Mtafiti, kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Theresia Masoi amesema hayo katika mkutano maalum wa masuala ya Kisayansi, utengaji wa bajeti ya kujiandaa kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Covid 19 na Kipindupindu.

Theresia amesema, Septemba 2023 kulikuwa na wagonjwa 1, 299 kati yao waliofariki ni 31 sawa na asilimia 2.6

Aidha amesema mboga mboga ambazo zimepandwa nyuma ya vyoo, au kumwagiliwa maji ambayo si salama ni chanzo pia cha ugonjwa wa kipindupindu.

“Kuna wale wasafiri wanaoenda mikoani, mabasi yanapita kwenye maeneo abiria wapate chakula, maeneo yale unakuta vyakula vilishaandaliwa, hamjui vimeandaliwaje, wakati mwingine vimepoa ni baridi, ni rahisi kupata ugonjwa wa kipindupindu, kipindupindu ni uchafu unaotokana na kinyesi, kuugua au kufa kwa kipindupindu ni uzembe,”amesema.

Aidha, amesema wanawake wanaongoza kuumwa kipindupindu kati ya wagonjwa walioripotiwa wanawake ni 314 wa umri wa miaka 15 hadi 49.

Habari Zifananazo

Back to top button