Mbogwe waadhimisha siku ya ukimwi duniani

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbogwe imeadhimisha siku ya Ukimwi duniani
ambapo watu 101 wamejitokeza kupima ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Katibu Tawala wa Mbogwe Jacob Julius akizungumza na HabariLEO leo Desemba Mosi amesema wanaume waliopima ni 71 na wanawake ni 30.

Advertisement

Aidha, amesema kwa mwaka jana zoezi la upimaji lilifanyika kwa siku tatu ambapo watu 23,000 waliopima na kati yao 700 walibainika kuwa na virusi.

“Kati ya watu 700 waliokutwa na virusi 300 walikua ni wanaume na wanawake ni 400,” amesema Jacob.

Aidha, anewapongeza wana Mbogwe kwa maamuzi yao ya kujitokeza na kupima afya zao kwa hiari.

Ameisihj jamii kutowanyanyapaa wale wanaobainika kuwa na virusi kwani kuwa na virusi sio mwisho wa maisha.

Jacob, amewataka wanaume kujitokeza kwa wingi zaidi kupima afya zao kwakuwa takwimu za mwaka jana zinaonesha wanawake walijitokeza wengi zaidi ndio maana idadi ya waliogundulika ilikuwa zaidi ya idadi ya wanaume.

Halmashauri ya Mbogwe inaendelea kuongeza juhudi za kupambana na VVU kwa kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuepuka mila na tamaduni zinazochangia maambukizi ya VVU kuongezeka.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *