MSANII kutoka kundi la WCB Wasafi, Mbwana Kilungi maarufu Mbosso Khan amesema endapo msanii mwenzake Aslay Isihaka atajiunga na kundi hilo, lebo ya kundi hilo itaongeza nguvu kwa kuwa ni msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuimba.
Mbosso amesema wasanii wengi wanauwezo mkubwa lakini endapo Aslay atasaini WCB yeye binafsi atafurahia ujio wake kwa sababu anapenda mafanikio ya wenzake na pia itasaidia kuimarisha zaidi lebo ya kundi hilo.
“Mi napenda sana wasanii wezangu wafaidike na vipaji vyao hivyo endapo Aslay atajiunga na WCB itaongeza kitu, Aslay sio wa mchezo ni msanii mkubwa na mwenye uwezo wa kuimba,”
Mbosso ameachia nyimbo tatu tu kwa mwaka huu amesema mwaka 2024 utakuwa mzuri kwake sababu utakuwa mwka wa kuachia nyimbo mwanzo mwisho.
“Naamini mwakani kwangu utakuwa mwaka mzuri sana katika muziki wangu sababu mwaka huu sijauandaa ila mwakani nimeandaa itakuwa ni kuachia tu ngoma mwaka mzima,” amesema Mbosso.